NEMUVIWA ni huduma ya Neno la Mungu kwa Vijana na watoto. Huduma hii imeanzia Tanzania Machi 17 mwaka 2012 inafanya kazi ndani na nje ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na inashirikiana na Huduma na Makanisa yote ya Kikristo ndani na nje ya Nchi. Makao makuu ya Huduma hiiyapo mtaa wa Majengo, kata ya Levolosi kwenye Jengo la Calvary Temple Kilombero Arusha Mjini.
Huduma hii ina malengo yafuatayo:-
a) Kuwafikia Watoto na Vijana kwa Injili ya Yesu Kristo Makanisani, Vituo vya Watoto wa Mtaani, Vituo vya Watoto yatima, na maeneo mengine yote walipo Vijana na Watoto.
b) Kuwakumbusha Wazazi jukumu lao la kuwalea Watoto na Vijana wao katika maadili ya Neno la Mungu,
c) Kuyakumbusha Makanisa kuandaa watumishi wa kuwafikia watoto na vijana kwa Neno la Mungu Makanisani, Vituo vya Watoto wa Mtaani, Vituo vya Watoto yatima,Mashuleni na maeneo mengine yote walipo Vijana na Watoto.
d) Kuwatafuta, kuwaandaa na kuwapeleka watumishi Makanisani, Vituo vya Watoto wa Mtaani, Vituo vya Watoto yatima, na maeneo mengine yote walipo Vijana na Watoto.
e) Kuaandaa na kuunda Mtandao wa waalimu wote wanaofanya huduma ya kufundisha kwa ukaribu wao.
f) Kuwawezesha hao Waalimu ili waweze kutimiza kusudi lao la kuujenga Ufalme wa Mungu kupitia kuwahudumia Watoto na Vijana.
g) Kuandaa Semina, Matamasha, Warsha, na Makongamano hasa Makanisani ili kuwabaini na kuwatambua watu wenye moyo na wito wa kuwafundisha Watoto na Vijana Neno la Mungu.
h) Kutilia mkazo kwa washirika na hata Wachungaji na Maaskofu kuona umuhimu wa Huduma hii ya Watoto na Vijana Makanisani, Vituo vya Watoto wa Mtaani, Vituo vya Watoto yatima,Mashuleni na maeneo mengine yote walipo Vijana na Watoto ili kutimiza agizo kuu.
i) Kutafuta, kuandaa mitaala itakayotumika kufundisha Watoto na Vijana Makanisani, Vituo vya Watoto wa Mtaani, Vituo vya Watoto yatima, Mashuleni na maeneo mengine yote walipo Vijana na Watoto.
j) Kufanya Tathimini na utafiti wa huduma Makanisani, Vituo vya Watoto wa Mtaani, Vituo vya Watoto yatima,Mashulenina maeneo mengine yote walipo Vijana na Watoto.
k) Kuwawezesha Watoto na Vijana kumtumikia Mungu na kuwaleta watu wengine kwa Yesu.
Kwa kifupi Hanya ndiyo maono ya huduma hii na tunapenda kuwashirikisha watu wote wenye moyo wa kupenda kawahudumia vijana na watoto waweze kushirikiana nasi kufanikisha huduma hii eidha kwa kwa kujiiunga kuwa mwanachama, kujitoa kwa hali na mali kufanikisha malengo ya huduma hii. Unaweza kujitolea kuwa mmoja ya wawezashaji kuwa kufundisha katika eneo lolote ambalo tumelitaja hapo juu au kwa kutuwezesha kwa kutupatia viteandea kazi kame vile vitabu, vifaa vya ofisini na kwa kutupatia mawazo ya kuboresha huduma hii.
Ofisi zetu zipo mtaa wa Majengo, kata ya Levolosi kwenye Jengo la Calvary Temple Kilombero Arusha Mjini.
Unaweza kuwasiliana nasi kwa Sanduku la Posta 1330, Arusha.
Barua pepe ni nemuviwa@gmail.com Simu: +255754 673 399, +255754 698 783 na +255756 241 011
2
Comments
Post a Comment